bantuleoBREAKING images

Discover Best bantuleoBREAKING Images of World

#food #travel #sports #news #may #friday

Hali ya usalama katika jiji la #Kinshasa uko chini ya udhibiti wa vikosi vya usalama vya serikali baada ya washambuliaji kadhaa, waliotambuliwa kuwa wanachama wa Vuguvugu jipya la #Zaire linaloongozwa na Christian Malanga ambaye ni mkongomani wa diaspora kujaribu kuteka baadhi ya ofisi za umma. Vikosi vya usalama vya serikali vimefanikiwa kuzima Jaribio la wanamgambo hao kabla ya kuleta madhara. Hapo kabla , wanamgambo hao walisikika wakisema kwenye video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa kuanzia leo "DRC haipo tena, na jina la zamani la nchi hiyo ndilo litatumika, ambalo ni Zaire". #RDC #tanzania #daresalaam #kenya #nairobi #uganda #kampala #drc #kinshasa #rwanda #kigali #burundi #bujumbura #mozambique #cabodelgado #niassa #nampula #malawi #lilongwe #somalia #Kismayo #comoro #moroni #zanzibar #bantuleo #bantuleoBREAKING

5/19/2024, 10:54:15 AM

Baada ya Ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mtibwa Sugar 3-1 na kufikisha pointi 71 ambazo hazitafikishwa na timu nyingine, #YoungAfricans ndio Mabingwa wapya msimu huu 2023/2024. Yanga pia imejihakikishia kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao wa 2023/2024. Aidha hii inakuwa mara ya tatu mfululizo kwa Yanga kutwaa taji la Ligi Kuu baada ya kuchukua katika misimu ya 2021/2022 na 2022/2023 na Sasa 2023/2024. Hilo linakuwa taji la 30 la Ligi Kuu kwenye historia ya Yanga ambayo inaongoza kuchukua ikifuatiwa na Simba iliyotwaa mara 22. Mpaka sasa, Yanga imeibuka na ushindi katika mechi 23, imetoka sare mara mbili na imepoteza michezo miwili tu. #tanzania #daresalaam #kenya #nairobi #uganda #kampala #drc #kinshasa #rwanda #kigali #burundi #bujumbura #mozambique #cabodelgado #niassa #nampula #malawi #lilongwe #somalia #Kismayo #comoro #moroni #zanzibar #bantuleo #bantuleoBREAKING

5/13/2024, 8:03:04 PM

Rais wa #Urusi Vladimir #Putin amembadilisha waziri wake wa ulinzi Sergei Shoigu na ambaye nafasi yake inachukuliwa na mtu asiye mwanajeshi, Andrey #Belousov, akitaja kupanda kwa matumizi ya kijeshi nchini humo na hitaji la "ubunifu." #Shoigu "ameondolewa" wadhifa wake wa Waziri wa Ulinzi kwa amri ya rais na kuteuliwa kuwa Katibu wa Baraza la Usalama la Urusi, msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov alisema Jumapili usiku. Shoigu pia atakuwa naibu wa Putin katika Tume ya Kijeshi-Viwanda ya Urusi, Peskov alisema, huku Nikolai Patrushev, Katibu wa wa Baraza la Usalama aliyepita, “atapangiwa kazi nyingine.” Belousov, ambaye hapo awali aliwahi kuwa naibu waziri mkuu wa kwanza, ni raia, ikimaanisha si mwanajeshi. na amechaguliwa na Putin kwa sababu ya hitaji la "ubunifu," Peskov alisema katika simu na waandishi wa habari, ambapo aliangazia bajeti inayoongezeka ya wizara, akisema ilikuwa inakaribia viwango vilivyoonekana mara ya mwisho wakati wa Vita Baridi. #tanzania #daresalaam #kenya #nairobi #uganda #kampala #drc #kinshasa #rwanda #kigali #burundi #bujumbura #mozambique #cabodelgado #niassa #nampula #malawi #lilongwe #somalia #Kismayo #comoro #moroni #zanzibar #bantuleo #bantuleoBREAKING

5/13/2024, 1:46:05 AM

Taarifa kutoka ndani ya #SimbaSC zinasema kiungo wake Clatous Chama, ameshapewa ofa mpya ambayo inaweza kumbakisha kiungo huyo lakini haitakuwa na presha yoyote ya kubadilika endapo Mzambia huyo atakuwa na ofa zingine kuishinda hiyo ya wekundu hao. . #Chama ambaye mkataba wake unafikia tamati mwisho wa msimu huu, mezani ana ofa kubwa mbili kutoka Yanga na Azam lakini mabosi wa klabu yake hawataki kuingia mtego wa kushindana na ofa hizo ikitaka kiungo huyo kufanya maamuzi ya mwisho. . “Sioni kama tutampa ofa kubwa zaidi ya hiyo ni uamuzi wake kuamua kama atakubaliana na hilo au vinginevyo kuna mambo mengi tunayapima kwenye hizi ofa ambazo tunawapa wachezaji wetu, kama ataona kuna ofa kubwa zaidi huko nje Simba haitashindana nazo,” alisema bosi huyo ambaye yumo kwenye bodi ya wakurugenzi wa Simba. #tanzania #daresalaam #kenya #nairobi #uganda #kampala #drc #kinshasa #rwanda #kigali #burundi #bujumbura #mozambique #cabodelgado #niassa #nampula #malawi #lilongwe #somalia #Kismayo #comoro #moroni #zanzibar #bantuleo #bantuleoBREAKING

5/11/2024, 12:31:49 PM

Leo kutoka bungeni Dodoma, aliyekuwa katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi, Katibu mkuu kiongozi na hivi sasa Mbunge wa bunge la Tanzania Bashiru Ally , amesema wizara ya utumishi inachelewesha kutoa vibali vya upandishaji vyeo vya wakufunzi wa vyuo vikuu nchini Tanzania. #Bashiru amesema tatizo hili linatokana na serikali ya Tanzania kuvifanya vyuo kama idara za serikali na sio taasisi nyeti za kimkakati zenye mazingira maalum na mahitaji maalum. Ameshauri vyuo vikuu vya umma vya Tanzania vinavyomilikiwa na serikali kumataifishwa "INTERNATIONALIZED" ili kumaliza matatizo kama hayo. #tanzania #daresalaam #kenya #nairobi #uganda #kampala #drc #kinshasa #rwanda #kigali #burundi #bujumbura #mozambique #cabodelgado #niassa #nampula #malawi #lilongwe #somalia #Kismayo #comoro #moroni #zanzibar #bantuleo #bantuleoBREAKING

5/8/2024, 6:02:51 PM

Rais wa Tanzania Samia Suluhu anatarajia kuzindua Mkakati wa serikali yake wa Nishati Safi ya Kupikia. Uzinduzi wa mkakati huo unaofanyika katika Ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Julius Nyerere JNICC leo tarehe 8 May, 2024 jijini Dar es Salaam. #tanzania #daresalaam #kenya #nairobi #uganda #kampala #drc #kinshasa #rwanda #kigali #burundi #bujumbura #mozambique #cabodelgado #niassa #nampula #malawi #lilongwe #somalia #Kismayo #comoro #moroni #zanzibar #bantuleo #bantuleoBREAKING

5/8/2024, 9:29:27 AM

Mtaalamu wa afya ya akili na masuala ya kijamii ameeleza kuwa kuwa kulingana na uzoefu anaoshuhudia anapokuwa kazini, idadi ya wanawake wanaojihusisha na vitendo vya usagaji Tanzania ni wengi kuliko wanaume wanaojihusisha na vitendo vya ushoga. Amesema asilimia kubwa ya wanaojihusisha vitendo vya usagaji na wanataka kuachana navyo, wanapoulizwa sababu ya kuingia katika vitendo hivyo hutoa sababu kuwa Vijana wa kiume ni wabinafsi sana kwenye mahusiano, pia wasagaji wanaamini Jinsia moja hufahamiana hisia vizuri zaidi kwa hiyo hujua wafanye nini ili kuridhishana. Sababu ya mwisho wanayoisema ni kuwa wanajua njia ya usagaji ni njia salama na hakuna uwezekano wa kupata mimba kwa hiyo pale atakapokuwa tayari kuolewa ataolewa tu kwakuwa hakuna uharibifu wowote wa kimaumbile atakaokuwa ameupata, tofauti na mashoga. Mtaalamu huyo ameshauri wazazi kuwa karibu na watoto wao na kuwa mfano wa watu wanaoishi maisha ya kujiheshimu kwa watoto wao. #tanzania #daresalaam #kenya #nairobi #uganda #kampala #drc #kinshasa #rwanda #kigali #burundi #bujumbura #mozambique #cabodelgado #niassa #nampula #malawi #lilongwe #somalia #Kismayo #comoro #moroni #zanzibar #bantuleo #bantuleoBREAKING

5/6/2024, 9:40:54 AM

Wabunge wa Bunge la Kenya wamepitisha hoja ya kumfuta kazi Mithika Linturi kama waziri wa Kilimo na Maendeleo ya Mifugo. Hii inakuja baada ya waziri huyo kutuhumiwa na bunge kushindwa kuwajibika kusimamia sekta ya kilimo na kuhusika na kashfa ya kifisadi ya mbolea feki iliyogawiwa kwa wakulima. Wabunge 149 walipiga kura kuunga mkono hoja ya kuanza kwa mchakato wa kuondolewa kwa Waziri huyo ambaye pia aliwahi kuwa seneta ya county ya Meru nchini Kenya. Na wabunge 36 walipiga kura kupinga hoja hiyo. Hatua hiyo inamaanisha kamati teule ya bunge iliyotajwa itaanza uchunguzi wake na kutoa ripoti ya mwisho. Wabunge walisikika kuimba kwa pamoja "LINTURI MUST GO" shighuli za buge zilipokuwa zikiendelea. Hoja ya kumuondoa Linturi ililetwa bungeni kwa mara ya kwanza na mbunge wa Bumula, Jack Wamboka akiwataka wabunge kuonyesha uongozi katika vita dhidi ya ufisadi kwa kumfukuza kazi Linturi la sivyo washindwe kuchaguliwa tena 2027. #tanzania #daresalaam #kenya #nairobi #uganda #kampala #drc #kinshasa #rwanda #kigali #burundi #bujumbura #mozambique #cabodelgado #niassa #nampula #malawi #lilongwe #somalia #Kismayo #comoro #moroni #zanzibar #bantuleo #bantuleoBREAKING

5/6/2024, 7:22:47 AM

Leo Tanzania 05 May 2024, Makamu Mwenyekiti-Bara wa Chama cha #CCM amejibu hoja zinazoendelea kutolewa katika mikutano mbalimbali ya kisiasa ya chama kikuu cha upinzania Tanzania cha #Chadema. Katika moja ya majibu yake amesema katiba mpya inayodaiwa na chadema haitakuwa jibu la mambo wanayoyataka wapinzania hao ikiwemo na ushindi katika uchaguzi. Amesisitiza kuwa dhamira njema ya Rais Samia Suluhu Hassan ndiyo hasa inayohitajika kwa sasa na siyo katiba mpya. Katika hilo Kinana ametolea mfano nchi jirani ambayo ina wapinzani waliopigania katiba mpya kupatikana na mara ilipopatikana wale walioipigania hawajawahi kushinda uchaguzi katika chaguzi zote sita baada ya kupatikana katiba mpya. #tanzania #daresalaam #kenya #nairobi #uganda #kampala #drc #kinshasa #rwanda #kigali #burundi #bujumbura #mozambique #cabodelgado #niassa #nampula #malawi #lilongwe #somalia #Kismayo #comoro #moroni #zanzibar #bantuleo #bantuleoBREAKING

5/5/2024, 10:44:25 PM